Loading

Utambukaji wa kipato. GRUMETI FUND na RAIZCORP

Fursa za kutengeneza kipato ni chache kwenye vijiji vinavyozunguka mapori ya akiba ya Ikorongoro - Grumeti. Asilimia kubwa ya kundi la wenye kufanya kazi ni wakulima. kiwango kidogo cha mvua na tembo wavamizi wa mazao ambavyo husababishwa na mabadiliko ya tabia nchi na kuishi karibu na wanyamapori huathiri hali ya maisha ya jamii hizi.

Unaweza kufikiri namna mtu anavyoweza kupoteza mazao yake kutokana na ukame na wanyama wenye njaa, kutavyomuacha na njia chache za kuingiza kipato. Ingawa sio kwama majangiri ndiyo mafukara, ni kawaida kwa mtu kujihusiha na shughuli hatari ya ujangiri ili ajipatie kipato pale anapokuwa hana mazao ya kuvuna.

Grumeti Fund imeungana na Raizcorp (Shirika lililobobea kwenye ukuzaji wa biashara lenye makao yake Afrika ya Kusini) ili kuwawezesha wajasiriamali wa vijiji vya pembezoni kuwa na biashara zenye tija.

Philip Kitasho ni Afisa Ukuzaji wa Biashara Vijijini. Amepitia mafunzo ya kina na Raizcorp na sasa ana wajibu wakushiriki maarifa yake kupitia uangalizi wa wajasiriamali na Madarasa Vijijini.

Uangalizi ni njia ya kuwawezesha wajasiriamali kwa kutoa mafunzo ya kibiashara kwa mtu-na-mtu inayowasaidia wajasiriamali kutumia stadi zao za biashara. Tangu kuanzishwa kwa mradi, 67% ya wajasiriamali kwenye programu hii wameongeza pato lao.

Madarasa Vijijini hujumuisha vipindi vya kila wiki kwa wajasiriamali chipukizi kwenye stadi za biashara na maendeleo binafsi. Programu ya madarasa vijijini imefikia washiriki 164, ambao 58% ni wanawake.

Ndani ya miezi 12 ijayo, Grumeti Fund imekusudia kufikia kima cha chini cha watu 300 kwenye madarasa vijijini na watu nane kupitia uangalizi. Pia, uzalishaji wa asali umeonekana kuwa shughuli nzuri ya kibiashara katika maeneo haya.

Grumeti Fund inahitaji $ 95,000 kuweza kufikia zaidi ya watu 300 kupita programu yake ya ukuzaji wa biashara kwa mwaka ujao.