Mkakati ni kila kitu kwenye masuala ya uzuia-ujangiri, ulinzi na usalama wa baadaye wa maeneo haya hutegemea mkakati. Kikosi cha intelijensia hufanya kazi kwa ukaribu na vitengo vya utekelezaji wa sheria vya serikali za mtaa ili kuzuia ujangiri. Pamoja nao ni kikosi cha oparesheni maalamu. Kikosi hiki cha askari mahiri hupokea taarifa na kuzishughulikia kukabili ujangiri.
Moja ya rasilimali muhimu kwenye kikosi cha oparesheni maalumu ni kitengo cha mbwa, chenye mbwa wanne na wanaowaongoza sita. Mbwa hawa wana uwezo wa kufuata na kugundua watu na nyamapori za magendo katika njia yoyote na kwa umbali mrefu. Timu nyingine ndani ya idara hujumuisha kitengo cha doria kinachotembea, kambi za skauti na maeneo ya kuangalizia mienendo hifadhini.
Sehemu muhimu ya Idara ya uzuia-ujangiri ni uwezo wa kuratibu sehemu zote zinazotembea. Utendaji kazi utegemea mfumo wa utambuzi wa kikoa wa EarthRanger. Kikiwa kwenye kituo cha oparesheni, mfumo huu (uliotengenezwa na Vulcan, Inc) hukusanya taarifa zote kutoka timu mbalimbali ndani ya hifadhi – kuanzia kwa watu hadi kwenye matukio – vyote huwekwa sehemu moja.
Bayonuani wako hatarini duniani kote. Timu zetu hapa Grumeti hufanya kazi kulinda bayonuai – kuanzia ujangiri wa nyamapori, pembe za ndovu na ujangiri wa faru, uchomaji wa mkaa na uchungaji haramu wa mifugo hifadhini. Timu hii haifanyi kazi pekee yake. Ni moja ya idara sita zifanyazo kazi ya kutunza uthamani wa ikolojia hii ya pekee na kuboresha maisha ya jamii za wenyeji kwa wakati mmoja.