Grumeti Fund inaadhimia kuchangia kuongeza idadi na kulinda spishi ya Faru weusi wa Afrika Mashariki walio hatarini kutoweka ndani ya Ikolojia ya Serengeti. Kwa kushirikiana na wadau wetu wa serikali ya Tanzania, tunafanikisha kuhamisha na kuwarejesha upya faru weusi kwenye makazi yao ya awali kaskazini mwa Tanzania.
Loading